Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 16:11-14 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Matendo ya Asa, toka mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha “Wafalme wa Yuda na Israeli.”

12. Katika mwaka wa thelathini na tisa wa ufalme wake, Asa alishikwa na ugonjwa wa miguu, akaugua sana. Lakini hata wakati huo, Asa hakumgeukia Mwenyezi-Mungu amsaidie, bali alijitafutia msaada kutoka kwa waganga.

13. Hatimaye Asa alifariki mnamo mwaka wa arubaini na moja wa utawala wake.

14. Alizikwa katika kaburi alilokuwa amejichimbia mwenyewe mwambani, katika mji wa Daudi. Walimlaza ndani ya jeneza lililokuwa limejazwa manukato ya kila aina yaliyotayarishwa na mafundi wa kutengeneza marashi, wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 16