Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 10:10-16 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Hao vijana wakamjibu, “Watu hao waliokuambia ‘Baba yako alitutwika mzigo mzito, lakini wewe utupunguzie,’ wewe waambie hivi: ‘Kidole changu kidogo cha mwisho ni kinene zaidi kuliko kiuno cha baba yangu.

11. Mzigo wa baba yangu ulikuwa mzito, lakini wangu utakuwa mzito zaidi. Baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa mijeledi yenye miiba.’”

12. Basi katika siku ya tatu Yeroboamu pamoja na watu wote wakarudi kwa Rehoboamu kama alivyokuwa amewaagiza.

13. Naye mfalme Rehoboamu akawajibu kwa ukali, akapuuza shauri la wazee,

14. na kufuata shauri la vijana wenzake. Basi akasema, “Baba yangu aliwatwika mzigo mzito, lakini mimi nitaufanya kuwa mzito zaidi. Baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa mijeledi yenye miiba”

15. Hivyo mfalme hakuwajali watu kwa sababu jambo hili lilisababishwa na Mungu ili Mwenyezi-Mungu atimize neno lake alilomwambia Yeroboamu, mwana wa Nebati kwa njia ya Ahiya wa Shilo.

16. Lakini watu wote wa Israeli walipoona kwamba mfalme hakuwajali walimwambia,“Tuna sehemu gani kwa Daudi?Hatuna urithi katika mwana wa Yese.Kila mmoja na arudi nyumbani kwake, enyi watu wa Israeli.Itunze nyumba yako mwenyewe, ee Daudi.”Hivyo watu wote wa Israeli wakarudi makwao.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 10