Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 1:14-17 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Solomoni alikusanya magari ya farasi na wapandafarasi; alikuwa na magari ya farasi 1,400, na wapandafarasi 12,000, ambao aliwaweka katika miji yenye vituo vya magari ya farasi na kwake katika Yerusalemu.

15. Mfalme Solomoni aliongeza fedha na dhahabu zikawa nyingi kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi zikapatikana kwa wingi kama mikuyu ya Shefela.

16. Farasi wa Solomoni walitoka Misri na Kilikia; wafanyabiashara wake waliwanunua huko.

17. Walinunua gari moja la farasi kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150 za fedha. Kisha waliwauzia wafalme wa Wahiti na Shamu farasi hao na magari.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 1