Agano la Kale

Agano Jipya

1 Samueli 2:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Halafu Hana aliomba na kusema:“Namshangilia Mwenyezi-Mungu moyoni mwangu.Namtukuza Mwenyezi-Mungu aliye nguvu yangu.Nawacheka adui zangu;maana naufurahia ushindi wangu.

2. “Hakuna aliye mtakatifu kama Mwenyezi-Mungu;hakuna yeyote aliye kama yeye;hakuna aliye mwamba kama Mungu wetu.

3. Acheni kujisifu,acheni kusema ufidhuli.Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu.Yeye huyapima matendo yote.

4. Pinde za wenye nguvu zimevunjika.Lakini wadhaifu wanaendelea kupata nguvu.

5. Wale ambao zamani walikuwa na chakula tele,sasa wanaajiriwa ili wapate chakula.Lakini waliokuwa na njaa,sasa hawana njaa tena.Mwanamke tasa amejifungua watoto saba.Lakini mama mwenye watoto wengi,sasa ameachwa bila mtoto.

6. Mwenyezi-Mungu huua na hufufua;yeye huwashusha chini kuzimunaye huwarudisha tena.

7. Mwenyezi-Mungu huwafanya baadhi wawe maskini,na baadhi wawe matajiri.Wengine huwashusha,na wengine huwakweza.

8. Huwainua maskini toka mavumbini;huwanyanyua wahitaji toka majivuni,akawaketisha pamoja na wakuu,na kuwarithisha viti vya heshima.Maana, minara ya dunia ni ya Mwenyezi-Mungu;yeye ameisimika dunia juu ya minara yake.

9. “Maisha ya waaminifu wake huyalinda,lakini maisha ya waovu huyakatilia mbali gizani.Maana, binadamu hapati ushindi kwa nguvu zake.

10. Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande;atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni.Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote;atampa nguvu mfalme wakeataukuza uwezo wa mteule wake.”

Kusoma sura kamili 1 Samueli 2