Agano la Kale

Agano Jipya

1 Samueli 15:18-29 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Mwenyezi-Mungu alipokutuma alikuambia, ‘Nenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hadi umewaua wote!’

19. Kwa nini basi, hukuitii sauti ya Mwenyezi-Mungu? Kwa nini mkakimbilia nyara na hivyo kutenda jambo ovu mbele ya Mwenyezi-Mungu?”

20. Shauli akajibu, “Nimetii sauti ya Mwenyezi-Mungu. Nilikwenda kule alikonituma Mwenyezi-Mungu; nimemleta Agagi mfalme wa Waamaleki, na nimewaangamiza kabisa Waamaleki.

21. Lakini watu walichukua nyara: Kondoo, ng'ombe na vitu vyote bora vilivyotolewa viangamizwe ili kumtambikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, huko Gilgali.”

22. Ndipo Samueli akamwambia,“Je, Mwenyezi-Mungu anapendelea zaididhabihu za kuteketezwa na matambiko,kuliko kuitii sauti yake?Tazama, kumtii yeye ni bora kuliko matambikona kumsikiliza kuliko kumtambikia mafuta ya beberu.

23. Uasi ni sawa na dhambi ya kupiga ramli,na kiburi ni sawa na uovu na kuabudu vinyago.Kwa sababu umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu,naye amekukataa kuwa mfalme.”

24. Shauli akamwambia Samueli, “Nimetenda dhambi. Nimeasi amri ya Mwenyezi-Mungu na amri yako, kwa sababu niliwaogopa watu, nikawatii wao.

25. Lakini sasa nakuomba, unisamehe dhambi yangu. Niruhusu nirudi pamoja nawe ili niweze kumwabudu Mwenyezi-Mungu.”

26. Samueli akamjibu: “Kamwe, siwezi kurudi pamoja nawe. Wewe umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme juu ya Israeli.”

27. Samueli alipogeuka ili aende zake, Shauli akashika pindo la vazi lake, nalo likapasuka.

28. Ndipo Samueli alipomwambia Shauli, “Tangu leo Mwenyezi-Mungu ameurarua ufalme wa Israeli kutoka kwako na atampa mtu mwingine miongoni mwa jirani zako aliye bora kuliko wewe.

29. Na Mungu ambaye ni utukufu wa Israeli hadanganyi, wala habadili wazo lake. Yeye si binadamu hata abadili mawazo.”

Kusoma sura kamili 1 Samueli 15