Agano la Kale

Agano Jipya

1 Samueli 13:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Shauli alikuwa na umri wa miaka kadha wa kadha alipoanza kutawala. Na alitawala Israeli kwa muda wa miaka … miwili.

2. Shauli aliwachagua Waisraeli 3,000. Kati yao, 2,000 alikuwa nao huko Mikmashi na katika nchi ya milima ya Betheli. Elfu moja aliwaweka huko Gibea katika eneo la Benyamini. Hao aliwaweka chini ya mwanawe Yonathani. Watu wengine wote waliobakia, aliwarudisha, kila mtu nyumbani kwake.

3. Yonathani alishinda kambi ya kijeshi ya Wafilisti huko Geba, na Wafilisti wote walisikia juu ya habari hizo. Hivyo Shauli alipiga tarumbeta katika nchi yote akatangaza, akisema, “Waebrania na wasikie.”

Kusoma sura kamili 1 Samueli 13