Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 8:8-13 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Shaharaimu aliwapa talaka wake zake wawili, Hushimu na Baara na baadaye alipata watoto wa kiume nchini Moabu.

9. Alimwoa Hodeshi, naye akamzalia wana saba: Yoabu, Sibia, Mesha, Malkamu,

10. Yeuzi, Sakia, na Mirma. Hawa wanawe wote walikuja kuwa wakuu wa koo.

11. Shaharaimu na mkewe Hushimu alipata wana wengine wawili: Abitubu na Elpaali.

12. Wana wa Elpaali walikuwa watatu: Eberi, Mishamu na Shemedi ambaye aliijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji kandokando yake.

13. Beria na Shema walikuwa miongoni mwa jamaa ambazo zilikuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na kuwafukuza wenyeji wa Gathi.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 8