Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 6:47-65 Biblia Habari Njema (BHN)

47. mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.

48. Ndugu zao wengine walipewa wajibu wa kuhudumia hema takatifu la nyumba ya Mungu.

49. Aroni na wazawa wake ndio waliokuwa wakitoa tambiko juu ya madhabahu ya tambiko za kuteketezwa na pia juu ya madhabahu ya kufukizia ubani. Walifanya kazi zote zilizohusika na mahali patakatifu sana ili kuifanyia Israeli upatanisho. Haya yote waliyafanya kulingana na maagizo aliyotoa Mose, mtumishi wa Mungu.

50. Wafuatao ndio wazawa wa Aroni: Aroni alimzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua,

51. Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Serahia,

52. Serahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu,

53. Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi.

54. Yafuatayo ndiyo makazi yao kulingana na mipaka yake: Wazawa wa Aroni katika jamaa ya Wakohathi kulingana na kura yao,

55. hao walipewa mji wa Hebroni katika nchi ya Yuda na malisho kandokando yake.

56. Lakini mashamba ya mjini pamoja na malisho yake alipewa Kalebu mwana wa Yefune.

57. Wazawa wa Aroni walipewa miji ya makimbilio: Hebroni, Libna pamoja na malisho yake, Yatiri na Eshtemoa pamoja na malisho yake,

58. Hileni na Debiri pamoja na malisho yake,

59. Ashani na Beth-shemeshi pamoja na malisho yake.

60. Katika eneo la kabila la Benyamini walipewa miji ya Geba, Alemethi na Anathothi pamoja na malisho ya miji hiyo. Miji yote waliyopewa kulingana na jamaa zao ilikuwa kumi na mitatu.

61. Miji kumi ya eneo la nusu ya kabila la Manase ilitolewa kwa sehemu iliyobaki ya ukoo wa Kohathi kwa kura kulingana na jamaa zao.

62. Ukoo wa Gershomu, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Naftali na katika kabila la Manase katika Bashani.

63. Vivyo hivyo, miji kumi na miwili katika kabila la Reubeni, na katika kabila la Gadi na katika kabila la Zebuluni ilipewa ukoo wa Merari kulingana na jamaa zao.

64. Kwa njia hii watu wa Israeli waliwapa Walawi miji ili waishi humo pamoja na malisho ya miji hiyo.

65. (Miji iliyotajwa majina hapa juu katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni na katika kabila la Benyamini iligawiwa kabila la Lawi kwa kura.)

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 6