Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 6:44-53 Biblia Habari Njema (BHN)

44. Ethani wa ukoo wa Merari, alikuwa kiongozi wa kundi la tatu la waimbaji. Ukoo wake kutokana na Lawi ni kama ifuatavyo: Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki,

45. mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,

46. mwana wa Amsi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri,

47. mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.

48. Ndugu zao wengine walipewa wajibu wa kuhudumia hema takatifu la nyumba ya Mungu.

49. Aroni na wazawa wake ndio waliokuwa wakitoa tambiko juu ya madhabahu ya tambiko za kuteketezwa na pia juu ya madhabahu ya kufukizia ubani. Walifanya kazi zote zilizohusika na mahali patakatifu sana ili kuifanyia Israeli upatanisho. Haya yote waliyafanya kulingana na maagizo aliyotoa Mose, mtumishi wa Mungu.

50. Wafuatao ndio wazawa wa Aroni: Aroni alimzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua,

51. Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Serahia,

52. Serahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu,

53. Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 6