Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 6:4-20 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Eleazari alimzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua,

5. Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi,

6. Uzi akamzaa Zerahia, Zerahia akamzaa Merayothi,

7. Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu,

8. Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi,

9. Ahimaasi akamzaa Azaria, Azaria akamzaa Yohanani,

10. na Yohanani akamzaa Azaria. (Azaria ndiye aliyefanya kazi ya ukuhani katika hekalu alilojenga mfalme Solomoni huko Yerusalemu).

11. Azaria alimzaa Amaria, Amaria alimzaa Ahitubu,

12. Ahitubu alimzaa Sadoki, Sadoki alimzaa Meshulamu,

13. Meshulamu alimzaa Hilkia, Hilkia alimzaa Azaria,

14. Azaria alimzaa Seraya, Seraya alimzaa Yehosadaki;

15. Yehosadaki alikwenda uhamishoni wakati Mwenyezi-Mungu alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa kuutumia mkono wa mfalme Nebukadneza.

16. Lawi alikuwa na wana watatu: Gershomu, Kohathi na Merari.

17. Kila mmoja wao pia alikuwa na wana. Gershomu aliwazaa Libni na Shimei;

18. Kohathi aliwazaa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli;

19. naye Merari aliwazaa Mahli na Mushi. Hizi ndizo jamaa za Walawi kulingana na koo zao.

20. Wafuatao ndio wazawa wa Gershomu kutoka kizazi hadi kizazi: Gershomu alimzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi, Yahathi akamzaa Zima,

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 6