Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 6:36-50 Biblia Habari Njema (BHN)

36. mwana wa Elkana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,

37. mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,

38. mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli.

39. Asafu, ndugu yake alikuwa upande wake wa kulia. Ukoo wake kutokana na Lawi: Asafu, mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,

40. mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya,

41. mwana wa Ethni, mwana wa Zera, mwana wa Adaya,

42. mwana wa Ethani, mwana wa Zima, mwana wa Shimei,

43. mwana wa Yahathi, mwana wa Gershomu, mwana wa Lawi.

44. Ethani wa ukoo wa Merari, alikuwa kiongozi wa kundi la tatu la waimbaji. Ukoo wake kutokana na Lawi ni kama ifuatavyo: Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki,

45. mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,

46. mwana wa Amsi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri,

47. mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.

48. Ndugu zao wengine walipewa wajibu wa kuhudumia hema takatifu la nyumba ya Mungu.

49. Aroni na wazawa wake ndio waliokuwa wakitoa tambiko juu ya madhabahu ya tambiko za kuteketezwa na pia juu ya madhabahu ya kufukizia ubani. Walifanya kazi zote zilizohusika na mahali patakatifu sana ili kuifanyia Israeli upatanisho. Haya yote waliyafanya kulingana na maagizo aliyotoa Mose, mtumishi wa Mungu.

50. Wafuatao ndio wazawa wa Aroni: Aroni alimzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua,

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 6