Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 6:25-38 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Wana wa Elkana walikuwa wawili: Amasai na Ahimothi.

26. Na hawa ndio wazawa wa Ahimothi: Ahimothi alimzaa Elkana, Elkana akamzaa Sofai, Sofai akamzaa Nahathi,

27. Nahathi akamzaa Eliabu, Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elkana.

28. Wana wa Samueli walikuwa wawili: Yoeli, mzaliwa wake wa kwanza, na Abiya, mdogo wake.

29. Na hawa ndio wazawa wa Merari kutoka kizazi hadi kizazi: Merari alimzaa Mali, Mali akamzaa Libni, Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,

30. Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaya.

31. Hawa ndio watu ambao mfalme Daudi aliwaweka wahudumu kama waimbaji katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, baada ya sanduku la agano kuwekwa ndani.

32. Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mkutano hadi wakati mfalme Solomoni alipojenga hekalu la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu. Waliutekeleza wajibu wao barabara, kwa zamu.

33. Zifuatazo ni koo za wale ambao walitoa huduma hizo: Ukoo wa Kohathi: Hemani, kiongozi wa kundi la kwanza la waimbaji, alikuwa mwana wa Yoeli. Ukoo wake kutokana na Israeli ni kama ifuatavyo: Hemani, mwana wa Yoeli, mwana wa Samueli,

34. mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa,

35. mwana wa Zufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,

36. mwana wa Elkana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,

37. mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,

38. mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 6