Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 6:21-30 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Zima akamzaa Yoa, Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera, Zera akamzaa Yeatherai.

22. Hawa ndio wazawa wa Kohathi kutoka kizazi hadi kizazi: Kohathi alimzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora, Kora akamzaa Asiri,

23. Asiri akamzaa Elkana, Elkana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,

24. Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli, Urieli akamzaa Usia, Usia akamzaa Shauli.

25. Wana wa Elkana walikuwa wawili: Amasai na Ahimothi.

26. Na hawa ndio wazawa wa Ahimothi: Ahimothi alimzaa Elkana, Elkana akamzaa Sofai, Sofai akamzaa Nahathi,

27. Nahathi akamzaa Eliabu, Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elkana.

28. Wana wa Samueli walikuwa wawili: Yoeli, mzaliwa wake wa kwanza, na Abiya, mdogo wake.

29. Na hawa ndio wazawa wa Merari kutoka kizazi hadi kizazi: Merari alimzaa Mali, Mali akamzaa Libni, Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,

30. Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaya.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 6