Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 4:35-43 Biblia Habari Njema (BHN)

35. Yoeli, Yehu (mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli.)

36. Eliehonai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya,

37. Ziza (mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri na mwana wa Shemaya).

38. Jamaa zao waliendelea kuongezeka kwa wingi sana. Hawa waliotajwa majina ni wakuu katika jamaa zao na koo zao ziliongezeka sana.

39. Walienea hadi kwenye lango la mji wa Gedori, upande wa mashariki wa bonde, ili kuwatafutia kondoo wao malisho.

40. Hapo, walipata malisho tele, tena mazuri sana na pia nchi ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani, kwani wenyeji wa nchi hiyo wa hapo awali walikuwa Wahamu.

41. Katika siku za mfalme Hezekia wa Yuda, watu hao waliotajwa majina yao walikwenda huko Gedori, wakaharibu hema za Wameuni waliokuwa wakiishi huko na kuwafukuza kabisa mpaka leo. Walifanya makao yao ya kudumu huko kwa sababu kulikuwa na malisho tele kwa ajili ya kondoo wao.

42. Watu wengine wa kabila la Simeoni wapatao 500 walikwenda mpaka kwenye mlima Seiri. Waliongozwa na Pelatia, Nearia, Refaya na Uzieli, wana wa Ishi.

43. Hapo waliwaua Waamaleki waliosalia baada ya kunusurika, na wakaishi huko mpaka leo.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 4