Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 3:9-24 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wengine waliozaliwa na masuria wake. Daudi alikuwa na binti pia, aliyeitwa Tamari.

10. Wazawa wa mfalme Solomoni: Solomoni alimzaa Rehoboamu, aliyemzaa Abiya, aliyemzaa Asa, aliyemzaa Yehoshafati,

11. aliyemzaa Yehoramu, aliyemzaa Ahazia, aliyemzaa Yoashi,

12. aliyemzaa Amazia, aliyemzaa Uzia, aliyemzaa Yothamu,

13. aliyemzaa Ahazi, aliyemzaa Hezekia, aliyemzaa Manase,

14. aliyemzaa Amoni, aliyemzaa Yosia.

15. Yosia alikuwa na wana wanne: Yohanani, mzaliwa wake wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia na wa nne Shalumu.

16. Yehoyakimu alikuwa na wana wawili: Yekonia na Sedekia.

17. Wana wa Yekonia aliyechukuliwa mateka na Wababuloni walikuwa saba: Shealtieli,

18. Malkiramu, Pedaya, Shenazari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.

19. Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Zerubabeli alikuwa na wana wawili: Meshulamu na Hanania, na binti mmoja, jina lake Shelomithi.

20. Zerubabeli pia alikuwa na wana wengine watano: Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-hesedi.

21. Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Yeshaya alimzaa Refaya, aliyemzaa Arnani, aliyemzaa Obadia, aliyemzaa Shekania.

22. Shekania alimzaa Shemaya. Wana wa Shemaya walikuwa sita: Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati.

23. Nearia alikuwa na wana watatu: Eliehonai, Hizkia na Azrikamu.

24. Eliehonai alikuwa na wana saba: Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 3