Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 27:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hii ndiyo orodha ya wakuu wa wazawa wa Israeli waliokuwa viongozi wa jamaa, na makamanda wa maelfu na mamia na maofisa wao waliomtumikia mfalme Daudi kuhusu zamu za kuingia na kutoka. Kila mwezi kila mwaka, kundi tofauti la watu 24,000 walilishika zamu ya kufanya kazi.

2. Yashobeamu mwana wa Zabdieli alikuwa kiongozi wa kikosi cha kwanza mnamo mwezi wa kwanza; kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

3. Yeye alikuwa mzawa wa Peresi, naye akawa mkuu wa makamanda wote wa jeshi katika mwezi wa kwanza.

4. Dodai alikuwa kiongozi wa kundi la pili katika mwezi wa pili. Kikosi chake kikiwa na wanajeshi 24,000.

5. Kamanda wa kundi la tatu likiwa na wanajeshi 24,000 alikuwa Benaya mwana wa Yehoyada, aliyekuwa kuhani mkuu.

6. Huyu ndiye Benaya aliyekuwa mtu shujaa katika kundi la watu 30, na kiongozi wa kundi hilo. Naye Amizabadi mwanawe, alikuwa kamanda.

7. Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa wa nne akiongoza kundi la nne lenye wanajeshi 24,000, na baada yake alimfuata Zebadia mwanawe.

8. Mwezi wa tano: Shamhuthi, Mwizrahi; alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.

9. Mwezi wa sita: Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoa; alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.

10. Mwezi wa saba: Helesi, Mpeloni, wa wana wa Efraimu; alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 27