Baadaye kulitokea tena vita huko Gathi ambako kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na kimo kikubwa, na vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake vidole ishirini na vinne. Yeye pia alikuwa mzawa wa majitu.