Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 2:7-17 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mwana wa Karmi, alikuwa Akari. Huyu aliwaletea Waisraeli taabu kwa sababu alijiwekea nyara zilizokuwa zimewekwa wakfu.

8. Ethani alikuwa na mwana mmoja, jina lake Azaria.

9. Wana wa Hesroni walikuwa Yerameeli, Ramu na Kelubai.

10. Ramu alimzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa kabila la Yuda.

11. Nashoni alimzaa Salma, Salma akamzaa Boazi,

12. Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.

13. Yese aliwazaa Eliabu, mwanawe wa kwanza, wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,

14. wa nne Nethaneli, wa tano Radai,

15. wa sita Osemu na wa saba Daudi.

16. Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.

17. Abigaili alimzaa Amasa ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 2