Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 2:48-54 Biblia Habari Njema (BHN)

48. Kalebu alikuwa na suria mwingine jina lake Maaka. Huyu alimzalia wana wawili: Sheberi na Tirhana.

49. Maaka alimzalia Kalebu wana; Shaafu mwanzilishi wa mji wa Madmana, na Sheva, mwanzilishi wa mji wa Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa pia na binti, jina lake Aksa.

50. Kalebu alikuwa na wazawa wengine pia kwa mkewe Efratha. Huri, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa na wana watatu: Shobali, mwanzilishi wa mji wa Kiriath-yearimu,

51. wa pili Salma, mwanzilishi wa mji wa Bethlehemu, na wa tatu Herefu, mwanzilishi wa mji wa Bethi-gaderi.

52. Shobali, mwanzilishi wa mji wa Kiriath-yearimu, alikuwa pia babu yao watu wa Haroe, na nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi,

53. pamoja na koo zifuatazo zilizoishi Kiriath-yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. (Wasorathi na Waeshtaoli walitokana na watu hao).

54. Salma, mwanzilishi wa mji wa Bethlehemu alikuwa babu ya Wanetofathi, Waatroth-beth-yoabu na nusu ya Wamenahathi yaani Wasori.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 2