Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 2:29-44 Biblia Habari Njema (BHN)

29. Abishuri alioa mke, jina lake Abihaili, naye akamzalia wana wawili: Abani na Molidi.

30. Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu; lakini Seledi alifariki bila watoto.

31. Apaimu alikuwa na mwana mmoja aliyeitwa Ishi. Ishi alimzaa Sheshani, na Sheshani akamzaa Alai.

32. Yada, nduguye Shamai, alikuwa na wana wawili: Yetheri na Yonathani. Lakini Yetheri alifariki bila watoto.

33. Yonathani alikuwa na wana wawili: Pelethi na Zaza. Wote hao ni wazawa wa Yerameeli.

34. Sheshani hakuwa na watoto wa kiume; alikuwa na binti tu. Hata hivyo, alikuwa na mtumwa wa Kimisri, jina lake Yarha.

35. Hivyo, Sheshani akamwoza Yarha mtumwa wake, mmoja wa binti zake, naye akamzalia mwana jina lake Atai.

36. Atai alimzaa Nathani, Nathani akamzaa Zabadi.

37. Zabadi akamzaa Eflali, Eflali akamzaa Obedi,

38. Obedi akamzaa Yehu, Yehu akamzaa Azaria,

39. Azaria akamzaa Helesi, Helesi akamzaa Eleasa,

40. Eleasa akamzaa Sismai, Sismai akamzaa Shalumu,

41. Shalumu akamzaa Yekamia, na Yekamia akamzaa Elishama.

42. Mzaliwa wa kwanza wa Kalebu, nduguye Yerameeli, aliitwa Mesha. Mesha alimzaa Zifu, Zifu akamzaa Maresha, Maresha akamzaa Hebroni.

43. Hebroni alikuwa na wana wanne: Kora, Tapua, Rekemu na Shema.

44. Shema alikuwa baba yake Rahamu na babu yake Rekemu. Rekemu nduguye Shema alimzaa Shamai,

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 2