Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 2:16-21 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.

17. Abigaili alimzaa Amasa ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.

18. Kalebu, mwana wa Hesroni, kutokana na wake zake wawili, Azuba na Yeriothi, aliwazaa Yesheri, Shaobabu na Ardoni.

19. Azuba alipofariki, Kalebu alimwoa Efratha aliyemzalia Huri.

20. Huri alimzaa Uri, naye Uri akamzaa Besaleli.

21. Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, dada yake Gileadi. Huyo alimzalia mwana jina lake Segubu.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 2