Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 2:11-24 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Nashoni alimzaa Salma, Salma akamzaa Boazi,

12. Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.

13. Yese aliwazaa Eliabu, mwanawe wa kwanza, wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,

14. wa nne Nethaneli, wa tano Radai,

15. wa sita Osemu na wa saba Daudi.

16. Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.

17. Abigaili alimzaa Amasa ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.

18. Kalebu, mwana wa Hesroni, kutokana na wake zake wawili, Azuba na Yeriothi, aliwazaa Yesheri, Shaobabu na Ardoni.

19. Azuba alipofariki, Kalebu alimwoa Efratha aliyemzalia Huri.

20. Huri alimzaa Uri, naye Uri akamzaa Besaleli.

21. Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, dada yake Gileadi. Huyo alimzalia mwana jina lake Segubu.

22. Segubu alimzaa Yairi ambaye alitawala miji mikubwa ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.

23. Lakini falme za Geshuri na Aramu ziliwashambulia na kuwanyanganya miji ya Haroth-yairi, Kenathi na vijiji vyake, jumla miji sitini. Hao wote walikuwa wazawa wa Makiri, baba yake Gileadi.

24. Baada ya Hesroni kufariki, Kalebu alimwoa Efratha, mjane wa Hesroni, baba yake. Efratha alimzalia Kalebu mwana jina lake Ashuri, aliyekuwa mwanzilishi wa mji wa Tekoa.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 2