Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 2:10-19 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Ramu alimzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa kabila la Yuda.

11. Nashoni alimzaa Salma, Salma akamzaa Boazi,

12. Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.

13. Yese aliwazaa Eliabu, mwanawe wa kwanza, wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,

14. wa nne Nethaneli, wa tano Radai,

15. wa sita Osemu na wa saba Daudi.

16. Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.

17. Abigaili alimzaa Amasa ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.

18. Kalebu, mwana wa Hesroni, kutokana na wake zake wawili, Azuba na Yeriothi, aliwazaa Yesheri, Shaobabu na Ardoni.

19. Azuba alipofariki, Kalebu alimwoa Efratha aliyemzalia Huri.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 2