Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 16:12-25 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda,maajabu yake na hukumu alizotoa,

13. enyi wazawa wa Abrahamu, mtumishi wake,enyi wazawa wa Yakobo, wateule wake.

14. Yeye Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu wetu;hukumu zake zina nguvu duniani kote.

15. Yeye hulishika agano lake milele,hutimiza ahadi zake kwa vizazi elfu.

16. Hushika agano alilofanya na Abrahamu,na ahadi aliyomwapia Isaka.

17. Alimthibitishia Yakobo ahadi yake,akamhakikishia agano hilo la milele.

18. Alisema: “Nitawapeni nchi ya Kanaani,nayo itakuwa mali yenu wenyewe.”

19. Idadi yenu ilikuwa ndogo,mlikuwa wachache na wageni katika nchi ya Kanaani,

20. mkitangatanga toka taifa hadi taifa,kutoka nchi moja hadi nchi nyingine,

21. Mungu hakumruhusu mtu yeyote awadhulumu;kwa ajili yao aliwaonya wafalme:

22. “Msiwaguse wateule wangu;msiwadhuru manabii wangu!”

23. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu, ulimwengu wote.Tangazeni kila siku matendo yake ya wokovu.

24. Yatangazieni mataifa utukufu wake,waambieni watu wote matendo yake ya ajabu.

25. Maana Mwenyezi-Mungu ni mkuu, anasifika sanaanastahili kuheshimiwa kuliko miungu yote.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 16