Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 14:9-15 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Wafilisti walifika wakaanza mashambulizi katika bonde la Refaimu.

10. Ndipo Daudi alipomwuliza Mungu shauri, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” Naye Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”

11. Basi, Daudi akaenda huko Baal-perasimu, akawashinda; halafu akasema, “Mungu amepita katikati ya adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji yaendayo kasi.” Kwa hiyo mahali hapo panaitwa Baal-perasimu.

12. Wafilisti walipokimbia, waliziacha sanamu za miungu yao huko, naye Daudi akatoa amri zote zichomwe moto.

13. Kisha Wafilisti walifanya mashambulizi katika bonde hilo kwa mara ya pili.

14. Safari hii, Daudi alipoomba shauri kwa Mungu, Mungu akamwambia, “Usiwashambulie kutoka hapa, ila zunguka na kuwashambulia kutoka mkabala na miti ya miforosadi, halafu washambulie kutoka huko.

15. Na mara utakaposikia vishindo vya gwaride kwenye vilele vya hiyo miforosadi, haya, toka uende vitani. Nitakuwa nimekwisha kukutangulia kulipiga jeshi la Wafilisti.”

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 14