Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 12:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hawa ni wanaume ambao walijiunga na Daudi huko Siklagi, alipokuwa hana uhuru wowote wa kutembea kwa sababu ya mfalme Shauli mwana wa Kishi; walikuwa miongoni mwa askari mashujaa waliomsaidia vitani.

2. Hao walikuwa watu wa kabila la Benyamini kama alivyokuwa Shauli. Walikuwa wapiga upinde hodari, na warusha mawe kwa kombeo kwa kutumia mikono yote, wa kulia na kushoto.

3. Kiongozi wao alikuwa Ahiezeri, aliyesaidiwa na Yoashi, wote wana wa Shemaa kutoka Gibea; wengineo ni: Yezieli na Peleti, wana wa Azmawethi, Beraka, Yehu kutoka Anathothi,

4. Ishmaya kutoka Gibeoni, mtu shujaa miongoni mwa wale thelathini na kiongozi wao pia pamoja na Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi kutoka Gedera,

5. Eluzai, Yeremothi, Bealia, Shemaria, Shefatia, Mharufi,

6. Elkana, Ishia, Azareli, Yoezeri, Yashobeamu kutoka ukoo wa Kora

7. na Yoela na Zebadia, wana wa Yerohamu, kutoka Gedori.

8. Tena, watu kutoka kabila la Gadi walijiunga na Daudi akiwa ngomeni kule nyikani. Hawa walikuwa askari wenye nguvu na uzoefu, hodari wa kutumia ngao na mkuki; wenye nyuso za kutisha kama simba na wepesi kama swala milimani.

9. Kiongozi wao mkuu alikuwa Ezeri, wa pili Obadia, wa tatu Eliabu,

10. wa nne Mishmana, wa tano Yeremia,

11. wa sita Atai, wa saba Elieli,

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 12