Agano la Kale

Agano Jipya

Yohane 7:41-53 Biblia Habari Njema (BHN)

41. Wengine wakasema, “Huyu ndiye Kristo!” Lakini wengine walisema, “Je, yawezekana Kristo akatoka Galilaya?

42. Maandiko Matakatifu yasemaje? Yanasema: ‘Kristo atatoka katika ukoo wa Daudi, na atazaliwa Bethlehemu, mji wa Daudi!’”

43. Basi, kukatokea mafarakano juu yake katika ule umati wa watu.

44. Baadhi ya watu walitaka kumtia nguvuni lakini hakuna aliyejaribu kumkamata.

45. Kisha wale walinzi wakarudi kwa makuhani wakuu na Mafarisayo; nao wakawauliza, “Kwa nini hamkumleta?”

46. Walinzi wakawajibu, “Hakuna mtu aliyepata kamwe kusema kama asemavyo mtu huyu!”

47. Mafarisayo wakawauliza, “Je, nanyi pia mmedanganyika?

48. Je, mmekwisha kumwona hata mmoja wa viongozi wa watu, au mmoja wa Mafarisayo aliyemwamini?

49. Lakini umati huu haujui sheria ya Mose; umelaaniwa!”

50. Mmoja wao alikuwa Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu. Basi, yeye akawaambia,

51. “Je, sheria yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza na kujua anafanya nini?”

52. Nao wakamjibu, “Je, wewe pia umetoka Galilaya? Haya, kayachunguze Maandiko Matakatifu nawe utaona kwamba Galilaya hakutoki kamwe nabii!”[

53. Basi, wote wakaondoka, kila mtu akaenda nyumbani;

Kusoma sura kamili Yohane 7