Agano la Kale

Agano Jipya

Yakobo 5:16-20 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.

17. Elia alikuwa binadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo mvua isinyeshe, nayo haikunyesha nchini kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.

18. Kisha akaomba tena, mvua ikanyesha kutoka angani na nchi ikatoa mazao yake.

19. Ndugu zangu, mmoja wenu akipotoka kuhusu ukweli, na mwingine akamrudisha,

20. fahamuni kwamba, huyo anayemrudisha mwenye dhambi kutoka njia yake ya upotovu, ataiokoa roho yake kutoka kifo, na dhambi nyingi zitaondolewa.

Kusoma sura kamili Yakobo 5