Agano la Kale

Agano Jipya

Yakobo 5:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Na sasa sikilizeni enyi matajiri! Lieni na kuomboleza kwa sababu ya taabu zitakazowajieni.

2. Mali zenu zimeoza, na nguo zenu zimeliwa na nondo.

3. Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Nyinyi mmejirundikia mali katika siku hizi za mwisho!

4. Hamkuwalipa mishahara watumishi waliofanya kazi katika mashamba yenu. Sikilizeni malalamiko yao! Kilio cha hao wanaovuna mashamba yenu kimefika masikioni mwa Bwana wa majeshi.

5. Mmeishi duniani maisha ya kujifurahisha na ya anasa. Mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa.

6. Mmemhukumu na kumuua mtu asiye na hatia, naye hakuwapingeni!

Kusoma sura kamili Yakobo 5