Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 8:15-19 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Kwa maana, hamkumpokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watumwa tena na kuwatia hofu, bali mmempokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watoto wa Mungu, na kwa Roho huyo, sisi tunamwita Mungu, “Aba,” yaani “Baba!”

16. Naye Roho mwenyewe anathibitisha na roho zetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu.

17. Basi, kwa vile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea baraka zote Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo pamoja na Kristo; maana, tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake.

18. Naona kuwa mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kamwe kama tukiyalinganisha na ule utukufu utakaodhihirishwa kwetu.

19. Viumbe vyote vinangojea kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake.

Kusoma sura kamili Waroma 8