Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 7:17-25 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Basi, si mimi hasa ninayefanya kitu hicho, bali ile dhambi inayokaa ndani yangu.

18. Najua kwamba hamna jema lolote ndani yangu mimi, kadiri ya ubinadamu wangu. Kwa maana, ingawa nataka kufanya jambo jema, siwezi kulitekeleza.

19. Yaani, badala ya kufanya lile jambo jema ninalotaka, nafanya lile baya nisilotaka.

20. Basi, kama ninafanya kinyume cha matakwa yangu, hii inamaanisha kwamba si mimi ninayefanya hayo, bali ni ile dhambi inayokaa ndani yangu.

21. Basi, nimegundua kanuni hii: Ninataka kufanya jema, lakini najikuta kwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua.

22. Ndani kabisa katika moyo wangu naifurahia sheria ya Mungu.

23. Lakini naona kwamba kuna sheria nyingine inayofanya kazi mwilini mwangu, sheria ambayo inapingana na ile inayokubaliwa na akili yangu. Hiyo inanifanya niwe mtumwa wa sheria ya dhambi ifanyayo kazi mwilini mwangu.

24. Maskini miye! Nani atakayeniokoa kutoka mwili huu unaonipeleka kifoni?

25. Shukrani kwa Mungu afanyaye hivyo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo!Hii basi, ndiyo hali yangu: Mimi binafsi, kwa akili yangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu ninaitumikia sheria ya dhambi.

Kusoma sura kamili Waroma 7