Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 3:7-20 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Labda utasema: “Ikiwa ukosefu wa uaminifu kwa upande wangu unamdhihirisha Mungu kuwa mwaminifu zaidi na hivyo kumpatia utukufu, basi singepaswa kuhukumiwa kuwa mwenye dhambi!”

8. Ni sawa na kusema: Tufanye maovu ili tupate mema! Ndivyo wengine walivyotukashifu kwa kutushtaki kwamba tumefundisha hivyo. Watahukumiwa wanavyostahili!

9. Tuseme nini, basi? Je, sisi Wayahudi ni bora kuliko wengine? Hata kidogo! Kwa maana nimekwisha bainisha hapo mwanzoni kwamba Wayahudi na watu wa mataifa mengine wote wako chini ya utawala wa dhambi.

10. Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:“Hakuna hata mmoja aliye mwadilifu!

11. Hakuna mtu anayeelewa,wala anayemtafuta Mungu.

12. Wote wamepotokawote wamekosa;hakuna atendaye mema,hakuna hata mmoja.

13. Makoo yao ni kama kaburi wazi,ndimi zao zimejaa udanganyifu,midomoni mwao mwatoka maneno yenye sumu kama ya nyoka.

14. Vinywa vyao vimejaa laana chungu.

15. Miguu yao iko mbioni kumwaga damu,

16. popote waendapo husababisha maafa na mateso;

17. njia ya amani hawaijui.

18. Hawajali kabisa kumcha Mungu.”

19. Tunajua kwamba sheria huwahusu walio chini ya sheria hiyo, hata hawawezi kuwa na kisingizio chochote, na ulimwengu wote uko chini ya hukumu ya Mungu.

20. Maana hakuna binadamu yeyote anayekubaliwa kuwa mwadilifu mbele yake Mungu kwa kushika sheria; kazi ya sheria ni kumwonesha tu mtu kwamba ametenda dhambi.

Kusoma sura kamili Waroma 3