Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 16:19-27 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Kila mtu amesikia juu ya utii wenu katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya.

20. Naye Mungu aliye chanzo cha amani hatakawia kumponda Shetani chini ya miguu yenu.Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.

21. Timotheo, mfanyakazi mwenzangu, anawasalimu. Hali kadhalika Lukio, Yasoni, na Sosipateri, wananchi wenzangu, wanawasalimu.

22. Nami Tertio, ninayeandika barua hii, nawasalimuni kwa jina la Bwana.

23. Gayo, mwenyeji wangu, pamoja na kanisa lote linalokutana kwake, anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto, wanawasalimu. [

24. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amina.]

25. Basi, sasa na tumsifu Mungu! Yeye anaweza kuwaimarisheni katika ile Habari Njema niliyohubiri juu ya Yesu Kristo, na katika ile siri iliyofunuliwa na ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyinyi zilizopita.

26. Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko ya manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirishwa kwa mataifa yote ili wote waweze kuamini na kutii.

27. Kwake Mungu aliye peke yake mwenye hekima, uwe utukufu kwa njia ya Yesu Kristo, milele na milele! Amina.

Kusoma sura kamili Waroma 16