Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 15:8-15 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;

9. ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Kwa hiyo nitakusifu miongoni mwa watu wa mataifa.Nitaziimba sifa za jina lako.”

10. Tena Maandiko yasema:“Furahini, enyi watu wa mataifa;furahini pamoja na watu wake.”

11. Na tena:“Enyi mataifa yote, msifuni Bwana;enyi watu wote, msifuni.”

12. Tena Isaya asema:“Atatokea chipukizi katika ukoo wa Yese,naye atawatawala watu wa mataifa;nao watamtumainia.”

13. Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

14. Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba nyinyi pia mmejaa wema, elimu yote, na mnaweza kushauriana nyinyi kwa nyinyi.

15. Lakini nimewaandikia hapa na pale katika barua hii bila woga, nipate kuwakumbusheni juu ya mambo fulani. Nimefanya hivyo kwa sababu ya neema aliyonijalia Mungu

Kusoma sura kamili Waroma 15