Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 15:29-33 Biblia Habari Njema (BHN)

29. Najua ya kuwa nikija kwenu nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.

30. Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo uletwao na Roho, mniunge mkono kwa kuniombea kwa Mungu.

31. Ombeni nipate kutoka salama miongoni mwa wale wasioamini walioko Uyahudi, nayo huduma yangu huko Yerusalemu ipate kukubaliwa na watu wa Mungu walioko huko.

32. Hivyo, Mungu akipenda, nitaweza kuja kwenu na moyo wa furaha, nikapumzike pamoja nanyi.

33. Mungu aliye chanzo cha amani na awe nanyi nyote! Amina!

Kusoma sura kamili Waroma 15