Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 15:19-26 Biblia Habari Njema (BHN)

19. kwa nguvu ya miujiza na maajabu, na kwa nguvu ya Roho wa Mungu. Basi, kwa kusafiri kila mahali, tangu kule Yerusalemu mpaka Iluriko, nimeihubiri kikamilifu Habari Njema ya Kristo.

20. Nia yangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njema popote pale ambapo jina la Kristo halijapata kusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.

21. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Watu wote ambao hawakuambiwa habari zake wataona;nao wale ambao hawajapata kusikia, wataelewa.”

22. Kwa sababu hiyo nilizuiwa mara nyingi kuja kwenu.

23. Lakini maadamu sasa nimemaliza kazi yangu pande hizi, na kwa kuwa kwa miaka mingi nimekuwa na nia kubwa ya kuja kwenu,

24. natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependa kuwaoneni nikiwa safarini kwenda Spania na kupata msaada wenu kwa safari hiyo baada ya kufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi.

25. Lakini, kwa sasa nakwenda kuwahudumia watu wa Mungu kule Yerusalemu.

26. Maana makanisa ya Makedonia na Akaya yemeamua kutoa mchango wao kuwasaidia watu wa Mungu walio maskini huko Yerusalemu.

Kusoma sura kamili Waroma 15