Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 14:9-16 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Maana Kristo alikufa, akafufuka ili apate kuwa Bwana wa walio hai na wafu.

10. Kwa nini basi, wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe, kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.

11. Maana Maandiko yanasema:“Kama niishivyo, asema Bwana,kila mtu atanipigia magoti,na kila mmoja atakiri kwamba mimi ni Mungu.”

12. Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu.

13. Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu au kumsababisha aanguke katika dhambi.

14. Katika kuungana na Bwana Yesu, nina hakika kwamba hakuna kitu chochote kilicho najisi kwa asili yake; lakini, mtu akidhani kwamba kitu fulani ni najisi, basi, kwake huwa najisi.

15. Kama ukimhuzunisha ndugu yako kwa sababu ya chakula unachokula, basi mwenendo wako hauongozwi na upendo. Usikubali hata kidogo chakula chako kiwe sababu ya kupotea kwa mtu mwingine ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake!

16. Basi, msikubali kitu mnachokiona kwenu kuwa chema kidharauliwe.

Kusoma sura kamili Waroma 14