Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 13:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima.

8. Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza sheria.

9. Maana, amri hizi: “Usizini; Usiue; Usitamani;” na nyingine zote, zimo katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”

10. Ampendaye jirani yake hamtendei vibaya. Basi, upendo ni utimilifu wa sheria.

Kusoma sura kamili Waroma 13