Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 12:13-21 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu.

14. Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani.

15. Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wenye kulia.

16. Ishini kwa kupatana vema nyinyi kwa nyinyi. Msijitakie makuu, bali jishughulisheni na madogo. Msijione kuwa wenye hekima sana.

17. Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote.

18. Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote.

19. Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”

20. Zaidi ya hayo, Maandiko yasema: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake.”

21. Usikubali kushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.

Kusoma sura kamili Waroma 12