Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 11:3-10 Biblia Habari Njema (BHN)

3. “Bwana, wamewaua manabii wako na kubomoa madhabahu yako. Ni mimi tu peke yangu niliyebaki, nao wanataka kuniua!”

4. Je, Mungu alimjibu nini? Alimwambia: “Nimejiwekea watu 7,000 ambao hawakumwabudu Baali.”

5. Basi, ndivyo ilivyo pia wakati huu wa sasa: Ipo idadi ya waliobaki ambao Mungu aliwateua kwa sababu ya neema yake.

6. Uteuzi wake unatokana na neema yake, na si kwa sababu ya matendo yao. Maana, kama uteuzi wake ungetegemea matendo ya watu, neema yake haingekuwa neema tena.

7. Sasa, je? Watu wa Israeli hawakukipata kile walichokuwa wanakitafuta; lakini wote walioteuliwa walikipata. Wengine walipumbazwa,

8. kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Mungu ameifanya mioyo yao kuwa mizito,na mpaka leo hii hawawezi kuona kwa macho yaowala kusikia kwa masikio yao.”

9. Naye Daudi anasema:“Karamu zao na ziwe mtego wa kuwanasa,waanguke na kuadhibiwa.

10. Macho yao yatiwe gizawasiweze kuona.Migongo yao ipindike kwa taabu daima!”

Kusoma sura kamili Waroma 11