Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 11:27-36 Biblia Habari Njema (BHN)

27. Hili ndilo agano nitakalofanya naowakati nitakapoziondoa dhambi zao.”

28. Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa maadui wa Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado ni marafiki wa Mungu kwa sababu ya babu zao.

29. Maana Mungu akisha wapa watu zawadi zake na kuwateua, hajuti kwamba amefanya hivyo.

30. Hapo awali nyinyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmepata huruma yake kutokana na kuasi kwao.

31. Hali kadhalika, kutokana na huruma mliyojaliwa nyinyi, Wayahudi wanamwasi Mungu sasa ili nao pia wapokee sasa huruma ya Mungu.

32. Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi wao ili apate kuwahurumia wote.

33. Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichunguziki, na njia zake hazieleweki! Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:

34. “Nani aliyepata kuyajua mawazo ya Bwana?Nani awezaye kuwa mshauri wake?

35. Au, nani aliyempa yeye kitu kwanzahata aweze kulipwa tena kitu hicho?”

36. Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, vyote vipo kwa uwezo wake na kwa ajili yake. Utukufu na uwe kwake hata milele! Amina.

Kusoma sura kamili Waroma 11