18. Ilikuwa tu baada ya miaka mitatu, ndipo nilipokwenda Yerusalemu kuonana na Kefa; nilikaa kwake siku kumi na tano.
19. Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana.
20. Haya ninayowaandikieni, Mungu anajua; sisemi uongo.
21. Baadaye nilikwenda katika tarafa za Siria na Kilikia.
22. Wakati huo, mimi binafsi sikujulikana kwa jumuiya za Wakristo kule Yudea.
23. Walichokuwa wanajua ni kile tu walichosikia: “Mtu yule aliyekuwa akitutesa hapo awali, sasa anaihubiri imani ileile aliyokuwa anajaribu kuiangamiza.”
24. Basi, wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.