Agano la Kale

Agano Jipya

Wafilipi 4:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.

2. Euodia na Suntike, nawaombeni na kuwasihi mpatane kama ndugu katika Bwana.

3. Nawe ndugu yangu mwaminifu, nakutaka uwasaidie akina mama hao, kwani wamefanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii pamoja nami na Klementi na wafanyakazi wenzangu wengine wote ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uhai.

4. Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini!

Kusoma sura kamili Wafilipi 4