Agano la Kale

Agano Jipya

Wafilipi 2:18-26 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Hali kadhalika nanyi mnapaswa kufurahi na kunishirikisha mimi furaha yenu.

19. Katika kuungana na Bwana Yesu ninalo tumaini kwamba nitaweza kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili nitiwe moyo kwa kupata habari zenu.

20. Sina mtu mwingine kama yeye ambaye anawashughulikieni kwa moyo.

21. Wengine wanashughulikia tu mambo yao wenyewe badala ya kuyashughulikia mambo ya Yesu Kristo.

22. Nyinyi wenyewe mwafahamu jinsi Timotheo alivyo thabiti; yeye na mimi, kama vile mtoto na baba yake, tumefanya kazi pamoja kwa ajili ya Injili.

23. Kwa hiyo natumaini kumtuma kwenu mara nitakapojua jinsi mambo yatakavyoniendea.

24. Na, ninatumaini katika Bwana kwamba nami pia nitaweza kuja kwenu karibuni.

25. Nimeona sina budi kumtuma kwenu ndugu yetu Epafrodito, ambaye ni mwenzangu kazini na vitani na ambaye ni mjumbe wenu aliyenisaidia katika mahitaji yangu.

26. Anayo hamu kubwa ya kuwaoneni nyinyi nyote, na amesikitika sana kwani nyinyi mmepata habari kwamba alikuwa mgonjwa.

Kusoma sura kamili Wafilipi 2