Agano la Kale

Agano Jipya

Wafilipi 2:17-23 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Hata ikiwa nitatolewa mhanga pamoja na imani yenu iliyo tambiko kwa Mungu, basi, nafurahi sana na kuwashirikisha nyinyi nyote furaha hiyo.

18. Hali kadhalika nanyi mnapaswa kufurahi na kunishirikisha mimi furaha yenu.

19. Katika kuungana na Bwana Yesu ninalo tumaini kwamba nitaweza kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili nitiwe moyo kwa kupata habari zenu.

20. Sina mtu mwingine kama yeye ambaye anawashughulikieni kwa moyo.

21. Wengine wanashughulikia tu mambo yao wenyewe badala ya kuyashughulikia mambo ya Yesu Kristo.

22. Nyinyi wenyewe mwafahamu jinsi Timotheo alivyo thabiti; yeye na mimi, kama vile mtoto na baba yake, tumefanya kazi pamoja kwa ajili ya Injili.

23. Kwa hiyo natumaini kumtuma kwenu mara nitakapojua jinsi mambo yatakavyoniendea.

Kusoma sura kamili Wafilipi 2