Agano la Kale

Agano Jipya

Waefeso 6:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.

2. “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani,

3. “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.”

4. Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.

5. Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na kutetemeka; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.

6. Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ili mjipendekeze kwao, bali tumikieni kwa moyo kama atakavyo Mungu kwa sababu nyinyi ni watumishi wa Kristo.

Kusoma sura kamili Waefeso 6