Agano la Kale

Agano Jipya

Waefeso 5:14-25 Biblia Habari Njema (BHN)

14. na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema:“Amka wewe uliyelala,fufuka kutoka kwa wafu,naye Kristo atakuangaza.”

15. Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi. Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima.

16. Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya.

17. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.

18. Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu.

19. Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na Zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.

20. Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

21. Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya heshima mliyo nayo kwa Kristo.

22. Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana.

23. Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake.

24. Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote.

25. Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake.

Kusoma sura kamili Waefeso 5