Agano la Kale

Agano Jipya

Ufunuo 11:16-19 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Kisha, wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,

17. wakisema:“Tunakushukuru ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu,uliyeko na uliyekuwako!Maana umetumia nguvu yako kuu, ukaanza kutawala!

18. Watu wa mataifa waliwaka hasira,lakini ghadhabu yako imefika,naam wakati wa kuwahukumu wafu.Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii,watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo.Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”

19. Kisha hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana hekaluni mwake. Kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.

Kusoma sura kamili Ufunuo 11