Agano la Kale

Agano Jipya

Ufunuo 11:12-17 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Kisha, hao manabii wawili wakasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni hapa juu!” Nao wakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui zao wakiwa wanawatazama.

13. Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu 7,000 wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.

14. Maafa ya pili yamepita; lakini tazama! Maafa ya tatu yanafuata hima.

15. Kisha, malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, “Sasa ufalme wa ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!”

16. Kisha, wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,

17. wakisema:“Tunakushukuru ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu,uliyeko na uliyekuwako!Maana umetumia nguvu yako kuu, ukaanza kutawala!

Kusoma sura kamili Ufunuo 11