Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 9:35-38 Biblia Habari Njema (BHN)

35. Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.

36. Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji.

37. Hapo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache.

38. Basi mwombeni mwenye mavuno atume wafanyakazi wavune mavuno yake.”

Kusoma sura kamili Mathayo 9